Zitto Sitogombea Urais wala Ubunge 2015
Zitto Sitogombea Urais wala Ubunge 2015 MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema hafikirii kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho wala ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015. Alisema mwaka 2015, ndio mwaka wa mwisho kujihusisha na siasa ambapo dhamira yake ni kutafuta chuo ambacho ataweza kufundisha masomo ya uchumi na maliasili. Bw. Kabwe aliyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalumu na gazeti hili siku chache baada ya viongozi 105 kutoka Vyuo Vikuu 30 nchini, kupendekeza majina ya wanasiasa wanaofaa kuwania urais mwaka 2015. Jina la Bw. Kabwe, lilishika nafasi ya pili katika mchujo huo ambapo Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba, alishika nafasi ya kwanza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwanasiasa aliyeshika nafasi ya tatu katika mchujo huo alikuwa Mbunge wa Ubungo, Dar es Salaam, Bw. John Mnyika (CHADEMA). "Hiki ni kipindi cha mwisho kwangu kujihusisha na s...